Sunday, September 2, 2012

USIKU WA M LAB SHOWCASE ZA TAMADUNI MUZIKI


         Stereo akiwapa puncho line mashabiki wake katika uzinduzi wa album yake pamoja na Nikki mbishi jana katika club ya  new msasani jijini Dar es Salaam.
         One incredible naye ni moja kati ya wasanii wanaotokea M lab chini ya producer duke aliwapangawisha mashabiki wake sana katika uzinduzi wa album ya nikki mbishi na stereo baada ya kumwambia Texas azime beat na kuanza kutumia beat ya mdomo.
        Mashabiki walikuwa wana furaha zaidi baada ya kumuona baba marco a.k.a Nikki mbishi katika stage jana maeneo ya msasani club katika uzinduzi wa mixtape pamoja na album kutoka m lab chini ya producer duke jijini Dar es salaam.
                                                                  Nikki mbishi
              Producer Duke akiongea machache na mashabiki wa hip hop waliofika katika uzinduzi huu wa album ya nikki mbishi na stereo jana maeneo ya msasani club jijini Dar es Salaam.
            Crew nzima ya m lab pamoja na producer wao waliamua kupamba stage na kushukuru mshabiki wao walioweza kufika katika uzinduzi wa mixtape pamoja na album ya Nikki mbishi na Stereo katika club new msasani jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment